Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika, Patrice Motsepe, ametangaza mpango wa kuzuru nchini Senegal katika wiki chache zijazo, akiwa na lengo la kuimarisha umoja na mshikamano barani Afrika kufuatia mivutano ya hivi karibuni.
Motsepe amesema wazi kuwa ujumbe wake mkuu ni kuunganisha Waafrika kupitia soka badala ya kuwagawa. “Tunawaunga mkono. Sisi sote ni Waafrika. Ujumbe huu huu niliutoa kwa Morocco. Wasenegali wengi wanaishi Morocco; hatutatumia mpira wa miguu kuwagawa watu. Lazima uwaunganishe watu,” alinukuliwa akisema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ziara hiyo inakuja katika kipindi nyeti kufuatia sakata la ubingwa wa AFCON 2025, ambalo limezua mjadala mkubwa na mvutano kati ya mataifa mbalimbali barani Afrika. Hatua ya Motsepe inalenga kupoza mihemko na kurejesha hali ya utulivu.
Kwa mujibu wa wachambuzi, kiongozi huyo anatumia soka kama daraja la kuunganisha mataifa, akisisitiza kuwa mchezo huo unapaswa kuwa chombo cha kuleta mshikamano. “Soka ni zaidi ya mchezo, ni jukwaa la kuimarisha undugu na ushirikiano wa Waafrika,” amesema mmoja wa wachambuzi wa michezo.
Aidha, Motsepe amegusia umuhimu wa mshikamano wa kijamii, akieleza kuwa Waafrika wanaoishi katika nchi jirani wanapaswa kulindwa na kuheshimiwa bila kujali tofauti za kisoka. “Maisha ya watu wetu na michezo yao haviwezi kutenganishwa, ni sehemu ya jamii moja,” aliongeza.
Ziara hiyo inatarajiwa kuwa na athari chanya katika kurejesha mahusiano ya kidiplomasia na kuimarisha mshikamano ndani ya CAF, huku wadau wakiamini kuwa ujumbe huo unaweza kusaidia kupunguza mvutano na kulinda taswira ya soka la Afrika.

