Kylian Mbappe anakiri kwamba “aliathiriwa” na malalamiko ya Olivier Giroud juu ya wachezaji wenzake wa Ufaransa kutompatia pasi lakini anasisitiza kuwa hataki kufanya kuwa suala kubwa.

Giroud alisema baada ya timu yake kuipiga Bulgaria katika mchezo wa kirafiki kwamba alikuwa hapokei mpira licha ya kukimbia kwenye maeneo hatari kwenye boksi.
Maoni hayo yalipokelewa tofauti na Mbappe na nyota wa Paris Saint-Germain anasema angependelea kama Giroud angezungumza naye kwa faragha badala ya kutoa malalamiko yake kwa waandishi wa habari.
“Nilizungumza na Olivier Giroud. Kila mtu anajua kilichotokea,” Mbappe alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
“Ni kweli kwamba niliathiriwa kidogo nayo. Lakini hatutafanya jambo hili kuwa kubwa kwa sababu tuko hapa kuiwakilisha Ufaransa, hilo ndilo jambo muhimu zaidi.
“Alichosema hakikunisumbua zaidi ya hapo, mimi ni mshambuliaji na nimekuwa na hisia hii mara 365 kwenye mchezo.
Les Bleus wataanza kampeni yao ya Euro 2020 na mchezo dhidi ya Ujerumani siku ya Jumanne.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.



Issa
Kaza buti
magdalena
Ndo changamoto za kazi izo
Hope mwaikuka
Mbaya sanaa hii