Anaandika Mwana Habari wa kituo cha Clouds Media Farhan Jr, Kwenye kurasa yake ya mtandaoni ya Instagram
Hii ni TOKYO, Japan 🇯🇵 na huyu Jamaa anaitwa Dan Orlowitz ni Mwandishi pia wa michezo huko akiandikia JAPAN TIMES na JT Sports, aliupenda sana uzi ya Yanga na akaulizia namna ya kuipata mtandaoni hatimae akaipata.

Jezi

Ilibidi aombe msaada kutoka kwa Mwandishi wa Ghana, Nuhu Adams amsaidie namna ya kuipata hii jezi, sio yeye peke yake ni wengi huwa nawaona wanaulizia sana huu uzi kupitia Twitter, alisema anaitaka jezi kwa gharama yoyote imfikie.

Imagine jezi imesafiri maili zaidi ya 7,012 kutoka Dar Es Salaam mpaka Mashariki ya mbali, nimefuatilia pia Yanga jezi zao zinanunuliwa sana Amerika ya Kati na Kusini, watu wanaagiza sana online.

Jezi

Nafikiri iko haja kwenye App yao waweke option ya kuuza jez mtandaoni ili iwe rahisi zaidi na zaidi kwao kwakuwa biashara hii inaonekana inapendwa sana duniani, nadhani ni kutokana na rangi zao pia.

Huo ni uzi wa Wananchi kwenye jiji la Tokyo, zipo picha nyingi pia kwenye majiji mengine makubwa! Naaam ni habari nzuri

Kwa Maelezo zaidi ya Uchambuzi na mwaswala ya kimichezo, Unaweza Kugusa Video hii hapo Chini 


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa