Tetesi zinasema,wakala wa Erling Braut Haaland, 21, Mino Raiola anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester City kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund msimu wa joto.
Mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, anataka kuhakikishiwa kwamba ni sehemu muhimu ya mipango ya Pep Guardiola kabla ya kuanza tena mazungumzo ya mkataba na Manchester City.
Tetesi zinasema, Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain, 28, kwa bei stahiki, huku klabu yake ya zamani ya Arsenal ikimtaka.

Tetesi zinasema, The Reds pia wameanza majadiliano ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto.
Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa England Phil Foden, 21, anakaribia kutia saini mkataba mpya Manchester City. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2024.
Tetesi zinasema, Manchester United wameungana na Chelsea na Juventus katikambio za kumsaka kiungo wakati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21.
Mlinzi wa Barcelona Clement Lenglet, 26, huenda akawa wa kwanza kuwasili Newcastle baada ya klabu hiyo kununuliwa hivi kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa akisemekana kuwa mchezaji klabu hiyo inamtaka.
Mchezaji wa Uhispania Hector Bellerin, 26, amedokeza kwamba hana nia ya kurejea Arsenal mkataba wake wa mkopo wa msimu mzima Real Betis utakapokamilika.

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, anatathmini hali ilivyo kabla ya kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake katika klabu ya Chelsea, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu.
Tetesi zinasema, Real Madrid wanapania kumrudisha mlinzi wa Tottenham Mhispania Sergio Reguilon, 24, katika uwanja wa Bernabeu kabla ya msimu ujao.
Leeds United wanakaribia kumsajili mshambuliaji kinda wa Espanyol Mhispania Mateo Joseph Fernandez 17. Leeds wamewasilisha dau la £450,000, lakini Espanyol wanataka pauni milioni moja (£1m).
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

