Yanga Wanataka Kufika Hatua ya Makundi Kwenye Michuano ya CAF

Klabu ya Yanga imeweka wazi mipango yake ya michuano ya kimataifa kwenye ligi ya klabu bingwa barani Afrika msimu unaotarajia kuanza hivi karibuni kuwa ,alemgo yao ni kufika hatua ya makundi msimu huu.

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Simon Patrick amesema kuwa kazi hiyo kwa upande wake sio kubwa pia mipango yao ya msimu ujao ni kufika hatua ya makundi kimataifa.

“Siwezi kusema ni kazi kubwa kwangu kwani hata kabla ya kuwa kwenye nafasi hii pia nilikuwa kiongozi lakini namshukuru Senzo kwani kanifundisha vitu vingi na kuifikisha Yanga pazuri. 

“Tumemaliza kazi sisi kama viongozi baada ya kupitia ripoti na kuifanyia kazi, tumeyafanyia kazi mapendekezo yote ya kocha kwa kufanya sajili mbalimbali hivyo kwa sasa kazi imebakia kwa Kocha. 

“Malengo yetu kwenye michuano ya kimataifa ni kufika hatua ya makundi na kwa ligi ya ndani ni kuchukua makombe yetu matatu na kocha analifanyia kazi hilo. 

“Kwanza mchezo ule tuliutumia kama mazoezi kwa kila mchezaji kuonyesha alichonacho na pia ulimsaidia kocha kuona alichowafundisha kwa muda mfupi na kwa sasa amerudi mazoezini hivyo jumamosi mtaiona Yanga ya tofauti.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.