Twiga Stars Yashinda Afrika Kusini.

Twiga Stars timu ya taifa wanawake ya Tanzania imefanikiwa kupata ushindi huko Afrika kusini kwenye michuano inayoendelea huko ya Cosafa.

Twiga wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya timu ya wanawake ya Comoros ambayo pia inashiriki michuano ya Cosafa inayofanyika nchini Afrika kusini.

twiga starsMagoli ya Twiga stars yamefungwa na Enekia Lunyamila aliefunga magoli mawili pamoja na Donisia Minja aliefunga goli moja katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Madibaz stadium,Pia kwenye mchezo huo mshambuliaji Enekia Lunyamila alifanikiwa mchezaji bora wa mchezo baada ya kufunga goli mbili katika mchezo.

Michuano hii inayojumuisha nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika Twiga stars wanakwenda kwenye michuano hii kama mabingwa watetezi baada ya kunyakua taji hili mwaka 2021 baada ya kuifunga Malawi goli moja kwa sifuri.

Baada ya ushindi wa leo Twiga stars wanajiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele na kuweza kutetea taji lake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.