Ahmed Ally: Azungumzia Suala la Kocha Simba.

Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amefunguka kuhusiana na mustakbali wa kocha ndani ya timu kutokana na taarifa tofauti tofauti zinazoendelea juu ya kocha wa mpya wa timu hiyo.ahmed allyKumekua na taarifa zinazoendelea juu ya klabu ya Simba kutafuta kocha mkuu licha ya mwalimu wasasa aliepewa timu Juma Mgunda kufanya vizuri na timu huku akiwa hajapoteza mchezo hata mmoja tangu akabidhiwe timu hiyo.

Hali hii imewafanya mashabiki wa timu hiyo kugawanyika pande mbili huku kuna upande ukiamini kocha wasasa Juma Mgunda anastahili kupewa mkataba wa kudumu klabuni hapo, Huku wengine wakiamini anahitajika mwalimu mwingine mkuu na Juma Mgunda abaki kama kocha msaidizi.

Hapo ndipo afisa habari wa timu hiyo Ahmed Ally alipoweka maelezo sawa baada ya kusema klabu hiyo ilikua na mchakato wa kutafuta kocha mkuu lakini klabu imesitisha mchakato huo kutokana na maendeleo mazuri ya kocha wasasa klabuni hapo kuvutia uongozi wa klabu hiyo.ahmed allyAidha Ahmed Ally amesisitiza kua kwasasa klabu imelenga kutafuta kocha wa viungo wa klabu hiyo ambaye aliondoka na benchi la ufundi liliondoka na aliekua kocha mkuu wa klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.