Joshua: Fury Panda Ulingoni na Mimi

Bingwa lazima awe mmoja tu katinga ngumi za uzani wa juu!! Haya yanaweza kuwa maneno ya bondia Anthony Joshua anapomuita Tyson Fury kupanda ulingoni apambane na yeye.

“Kama kweli unataka kusema kuwa wewe ninamba moja, njoo upigane na mimi”
-Anthony Joshua

Baada ya Fury kumtandika Deontay Wilder na kuchukua mkanda wa ubingwa wa WBC, sasa mataji ya upingwa yapo Uingereza wakati Joshua akiwa anashikilia mataji ya IBF, WBA na WBO kutoka kwa Andy Ruiz Jr mwezi Disemba.

Anthony Joshua amefunguka kuwa Furry hawezi kujiita yeye ni bingwa wa dunia bila kukutana naye ulingoni. Joshua anasisitiza kuwa mpaka amchape yeye ndiyo anweza kujiita bingwa!

“Kama kweli unataka kusema kuwa wewe ninamba moja, njoo upigane na mimi. Tupambane. Ninayo mikanda yote ya ubingwa inayosalia na inaleta maana hilo tu likifanyika”

-Anthony Joshua

Fury tayari alikuwa amekubali kupambana na Deontay Wilder kwa mara ya tatu, mechi iliyotarajiwa kupiganwa oktoba, wakati huo Joshua anatarajiwa pia kuingia pambano la lazima dhidi ya Kubrat Pulev kulinda ubingwa wake.

Acha ujumbe