Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Newcastle wamewasiliana na wawakilishi wa kiungo wa Ufaransa anayechezea timu ya Leicester City, Wesley Fofana kuhusu uwezekano wa uhamisho katika dirisha la uhamisho wa mwezi wa Januari.

Kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot amehusishwa na uhamisho wa Newcastle , huku klabu hiyo ya Serie A ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwezi Januari ili kuweza kutafuta fedha za kumnunua kiungo wa kati wa Monaco na raia wa Ufaransa Aurelien Tchouameni au kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 24.

Tetesi zinasema, Monaco wameweka bei ya euro milioni 60 kwa kijana mwenye umri wa miaka 20 Tchouameni, huku Real Madrid, pamoja na Manchester City, Chelsea na Liverpool wakimtaka mchezaji huyo.

Barcelona wako makini kumuachilia Philip Coutinho katika kipindi cha dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku Liverpool ikiwa tayari kumrejesha tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 katika uwanja wa Merseyside.

 

Coutinho Awekwa Sokoni na Barcelona.

Tetesi zinasema, Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers ndiiye mtu wa kwanza anayefikiriwa kuchukuliwa na wamiliki wa klabu ya Newcastle iwapo wataamua kumfuta kazi meneja wa sasa Steve Bruce.

Real Madrid wanania ya kusaini mkataba na mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, 28. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani unamalizika mwishoni mwa msimu huu na ataongeza uzoefu wake kwa klabu hiyo ya Uhispania.

Phil Foden amesitisha mpango wake wa kusaini mkataba na Manchester City wenye thamani ya karibu pauni milioni 50, huku makubaliano ya kiungo huyo ya miaka sita yakimuwezesha kulipwa pauni 150,000 kila wiki.

Tetesi zinasema, Arsenal wanajianda kwa dau la euro milioni 30 kwa ajili ya winga wa klabu ya Club Bruges mwenye umri wa miaka 22 Mholanzi Noa Lang.

Manchester United wanataka kufufua juhudi zao za kusaini mkataba na kiungo mlinda lango wa Sevilla Mfaransa Jules Kounde ambaye pia bado analengwa na Chelsea.

 

Barcelona wamemuongeza mkataba mpya wa miaka mitano kiungo wa kati wa Uhispania Pedri ambao utaendelea hadi 2026 na release close ya euro bilioni moja.

Paris St-Germain huenda wakamnunua mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Tetesi zinasema, Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone alijaribu kumsajili Lionel Messi, 34, msimu wa joto na alimpa kibarua hicho mshambuliaji Luis Suarez kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kujiunga na klabu hiyo kabla ya kuhamia Paris St-Germain.


PIGA MKWANJA NA LA ROUGE

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.