Mchezaji nyota wa klabu ya Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang ametangaza kustaafu soka la kimataifa na amethibitisha kuwa hataiwakilisha tena taifa la Gabon ila bado ataendelea kucheza soka la kulipwa.

Aubameyang ambaye awali alliwa kuiwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa kwa ngazi za vijana, kabla ya kuamua kurudi Africa na kwenda kuiwakilisha timu ya taifa ya Gabon. Pia amefanikiwa kuliongoza taifa la Gabon kwenye mashindano mbali mbali ikiwemo mashindano ya Olympic jijini London mwaka 2012.

Aubameyang

Aubameyang aliachia waraka ambao ulisomeka, “baada ya miaka 13 ya kuiwakilisha nchi yangu, natangaza kwamba naachana na soka la kimataifa. Ningependa kuwashukuru watu wa Gabon na wale wote ambao walinisaidia kwenye kipindi kizuri na kibaya.

“Nitahifadhi kumbukumbu nyingi nzuri, kama siku ya kwanza kucheza au siku niliyorudi kutoka Nigeria na Ballon d’or ya Afrika, kushirikiana na watu ni kipindi kisichosahaulika.

“Namshukuru raisi wetu Ali Bongo Ondimba ambaye amekuwa akinisapoti na mara zote amekuwa akifanya kazi ya kuendeleza soka kwenye nchi yetu. Pia ningependa kuwashukuru makocha wangu wote, wafanyakazi na wachezaji wote ambao nimekuwa nao kwenye maisha yangu ya soka.

“Mwishoni, namshukuru baba yangu ambaye alinipa shuku ya kufanya kama yeye, natumai mimepa sifa ya kuvaa jezi ya taifa lake.”

Mwaka 2015 Aubameyang alikuwa ni mchezaji wa kwanza kutokea Gabon kushinda mchezaji bora wa mwaka Afrika.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa