Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amedai kuwa ni mapema sana kuzungumzia hatima yake ya kuhusu maisha yake ya baadae kama kocha wa Uingereza baada ya kukubali kufungwa katika fainali ya Euro 2020.
Katika mechi iliyoshuhudia Italia walio kwenye moto wa kushambulia na kutawala sana eneo la Kati, Kocha Southgate alionekana kuishiwa ujanja na kushuhudia vijana wake wakikosa ubingwa kwenye hatua ya matuta.
Akizungumza na waandishi wa habari, Gareth alidai kuwa michuano ya Euro 2020 imekuwa chachu kubwa ya kuunganisha Uingereza na anahisi kama timu kwa pamoja wamefanya vitu vingi sana toka achukue timu hii mwaka 2017.
Alipoulizwa kuhusu hatima yake, Southgate alidai kuwa anatamani akapumzike na angalie marejeo na kutathmini mechi zote za michuano hii ili arudi imara kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia mwakani pale Qatar.
Licha ya hilo, Gareth alikubali kubeba mzigo wa lawama wa wachezaji wake kufuatia baadhi ya vijana wadogo, Sancho, Rashford na Saka ambao walikosa penati kwa ukweli kuwa yeye ndiye aliyechagua watakaopiga penati na kiujumla kama timu ndiyo iliyopoteza sio mchezaji mmoja mmoja.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!