Renato Sanches: "Niko Tayari" - Anatimba Arsenal?

Kiungo wa kati wa Lille Renato Sanches amezungumzia kuhusishwa kwake kwa hivi majuzi na klabu ya Arsenal kwa kutangaza kuwa ‘yuko tayari’ kuondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa.

Kiungo huyo wa Ureno kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kutaka kurejea katika klabu moja kubwa ya Ulaya baada ya kufanya vyema nchini Ufaransa, ambako akiwasaidia Lille kushinda taji la Ligue 1 msimu uliopita.

Arsenal na Liverpool zimekuwa ni timu mbili pekee barani Ulaya zinazohusishwa kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ama katika dirisha la uhamisho la Januari au msimu wa joto.

Renato Sanches
Renato Sanches

Sasa katika mahojiano, Sanches amezungumzia uvumi huo kwa kusema:

“Labda Milan na Arsenal wana nia lakini sijui. Nilizungumza na wakala wangu, najua ni klabu gani zinaniita lakini siwezi kusema sawa kwa sasa.”

“Lakini najua niko tayari. Ikiwa ofa itaingia, nitajua ni nini kinachonifaa zaidi.”

Baada ya kuhamia Bayern Munich kutoka Benfica akiwa na umri wa miaka 18 kwa takriban £31.5m, Sanches alipata shida kuzoea ligi ya Ujerumani na alitolewa kwa mkopo kwa Swansea City mnamo 2017.

Kufuatia kipindi kigumu cha mkopo huko Wales, Lille wakamsajili kutoka Bayern msimu wa joto wa 2019 kwa karibu £18m.

Lille kwa sasa wanapambana kuwepo nafasi10 bora za msimamo wa Ligue 1 msimu huu, na inafahamika kuwa wako tayari kumuacha Sanches aondoke ikiwa ofa sahihi itawasilishwa kwa ajili yake na mkataba wake ukiwa unamalizika msimu wa joto wa 2023.


Vuna Mkwanja na Keno

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe