Serikali ya Uingereza imefanya mabadiliko kwenye leseni ya klabu ya Chelsea ya uendeshaji ili kuweza kuinusuru klabu hiyo kutoka kwenye mikono ya Roman Abramovich baada ya kumuwekea vikwazo.
Wiki iliyopita tajiri huyo alikuwa ni miongoni mwa warusi waliyowekewa vikwazo, na mali zake kushikiliwa na serikali kutokana na kuwa na uhusiano na rais wa urusi Vladimir putin, na siku ya jumamosi Roman alivuliwa ukurugenzi wa klabu ya Chelsea na bodi ya ligi kuu.

Roman Abramovich alijaribu kuiweka sokoni klabu hiyo kwa kiasi cha £3bilion, lakini hakufanikiwa mpaka serikali ilipozuia mali zake ikiwemo klabu hiyo na kuiwekea vikwazo.
Baada ya majadiliano ya siku mbili kati ya wawakilishi wa klabu ya Chelsea na wawakilishi wa serikali wameipatia klabu hiyo ahueni baada ya serikali kuamua kuipitia upya leseni klabu hiyo na kupunguza baadhi ya vikwazo huku wakiruhusu Chelsea kutumia kiasi cha ziada £110million.
Pesa za haki ya matangazo ambazo awali zilizuiliwa sasa zimefunguliwa, na Chelsea wataendelea kulipa kiasi cha £28million kila mwezi kama mishahara na matumizi mingine.
Chelsea walikuwa wanapokea kiasi cha £35milioni kutoka EPL na UEFA kama haki ya matangazo ambacho walizuia kukitumia kwenye masharti ya vikwazo vya awali ambapo sasa wameruhusiwa kukitumia. Pia wameruhiswa kupokea kiasi £39milion kama wataweza kumaliza nafasi ya tatu na £36milioni kama wakitetea ubingwa wa Ulaya.
Pia wameongezewa bajeti ya mechi kwa siku kutoka £500,000 hadi £900,000 wakati qaliwekewa ukomo wa £20,000 kwa ajiri ya gharama za usafiri pia inatarajiwa kuongezwa ikiwa wataweza kuindoa Lille.
Msemaji wa idara kidijitari, utamaduni michezo na habari alisema, “tulisema kuwa tutakaa na chelsea ili kuelewa ni nini kinahitajika kuruhu ili waendelee kucheza na kupunguza matatizo yao kwenye ligi na mashabiki.”
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.


