Tetesi zinasema, Manchester United wanazidi kujiamini kuwa wanaweza kumteua kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino kama meneja wao wa kudumu katika majira ya joto.

Manchester City wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 tayari kuwa na mkataba unaoendelea hadi 2025.

Beki wa kati wa Real Madrid Mbrazil Eder Militao, 24, anawaniwa na Chelsea msimu wa joto kama mbadala wa Mjerumani Antonio Rudiger, 28, na Mdenmark Andreas Christensen, 25, ambao wote wanaweza kuondoka wakiwa huru mwishoni mwa msimu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema klabu hiyo itafanya kila iwezalo kumsajili tena mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30 Alexandre Lacazette kutoka Arsenal msimu wa joto.

Tetesi zinasema, Tottenham na Juventus zote zinavutiwa na winga wa Roma mwenye umri wa miaka 22 Nicolo Zaniolo.

Mabingwa wa Italia Inter Milan na wapinzani wao wa jiji la AC Milan wako tayari kumenyana na Real Madrid katika usajili wa beki wa kati wa Arsenal wa chini ya miaka-21 William Saliba, 20, ambaye yuko Marseille kwa mkopo.

Tetesi zinasema, Real Madrid wanafikiria kutumia kipengele cha kumnunua tena katika mkataba wa Sergio Reguilon ili kumsajili tena beki huyo wa miaka 25 kutoka Tottenham katika msimu wa joto.

Barcelona wanasemekana wamebainisha Manchester United na Juventus kama vilabu vinavyotaka kumsajili winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye atakuwa mchezaji huru msimu wa joto.

 

Ousmane Dembele Aachwa Kwenye Kikosi cha Barca

Tetesi zinasema, Derby County wamekubali ofa ya £600,000 ya Aston Villa la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Ireland Kaskazini wa miaka 16 Omari Kellyman.

Klabu ya Lille nchini Ufaransa imekataa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa zamani Jack Wilshire ambaye anasalia kuwa mchezaji huru baada ya kutolewa na Bournemouth mwezi Mei mwaka jana.

Mlinzi wa Blackburn Rovers Darragh Lenihan, 27, anatakiwa klabu ya Ligi ya Marekani New York Red Bulls na inasemekana wanajiandaa kuwasilisha ofa nono kumnunua kiungo huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa