Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuingia mkataba na shirika la watoto duniani lijulikanalo kama UNICEF jambo hilo ambalo limetangazwa leo mapema na Rais wa klabu hiyo Eng Hersi Said.
Katika mkutano uliofanyika kwenye Hotel ya Serena huku wanahabari wakialikwa ambapo klabu hiyo ilisaini mkataba na shirika hilo ambalo lrngo kubwa likiwa ni kutengeneza uelewa kwa jamii namna ya kujikinga na gonjwa la Uviko 19 pamoja na Ebola.
Katika hafla hiyo iliyokua ikiongozwa na Rais wa klabu ya Yanga pamoja na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine wameweza kueleza kwanini shirika hilo limewachagua wao kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii badala ya vilabu vingine.
“Ni heshima kubwa kuingia mkataba na UMOJA WA MATAIFA ni kwa mara ya kwanza katika historia kwa vilabu vya hapa Afrika Mashariki, pia ushirikiano na UNICEF umejengwa katika falsafa ya Klabu ya kusaidia jamii. “Tunajulikana kama Timu ya Wananchi.
“Kutokana na uimara wetu katika utoaji wa taarifa za fedha UNICEF wamevutiwa kufanya kazi na sisi. UNICEF haiwezi kufanya kazi na wababaishaji. Tumekuwa wa wazi kwenye mapato na matumizi. Hivyo wameona sisi ni sehemu sahihi ya wao kuleta miradi yao kwetu.” Alisema Inginia Rais wa klabu.
“Young Africans inatoa huduma ya burudani kwa Jamii. Lakini hatuwezi kutoa burudani kama Jamii tunayotegemea inasakamwa na maradhi. Hivyo tuna wajibu wa kutoa elimu kwa kuunga mkono mipango ya serikali kupambana na maradhi”
Rias wa klabu ya Yanga ameeleza kwanini shirika hilo limeamua kuwapa dhamana wananchi na sio klabu nyingine huku shirika hilo pia wamesema wanaamini kupitia klabu hiyo wanaweza kufikia watu zaidi ya milioni 25 nchini Tanzania na wakapata uelewa wa kutosha juu ya Uviko 19 pamoja na Ebola.

