Azam Fc Mbioni Kumtimua Lavagne.

Klabu ya Azam Fc ipo mbioni kumtimua kocha wake mkuu Dennis Lavagne raia wa Ufaransa baada ya kupata matokeo ya kutoridhisha hivi karibuni na kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo.

Taarifa za ndani kutoka klabu ya Azam  zinaeleza klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kuvunja mkataba na kocha huyo ambaye alitambulishwa mwanzaoni mwa mwezi wa tisa na kufikia mwezi wa kumi anakaribia kufungashiwa virago. azam fcKocha huyo ameiongoza klabu ya Azam Fc katika michezo minne ya ligi kuu  akifungwa miwili na kushinda miwili huku akitolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika na viongozi wa klabu hiyo kuona kocha Lavagne hawezi kuwafikisha nchi ya ahadi.

Azam Fc ambao wamepoteza mchezo jana kwa kufungwa na klabu KMC inaelezwa ndo sababu kubwa kwa viongozi wa klabu hiyo kutaka kusitisha mkataba wa kocha huyo.azam fcTaarifa zinaeleza timu hiyo itabakichini ya kocha Badru pamoja Kali Ongala ambae ni kocha wa washambuliaji wa klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.