Morocco Yafungua Kesi FIFA Dhidi ya Senegal Kuhusu Kombe la AFCON 2025

Morocco inatarajiwa kuwasilisha malalamiko rasmi mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA dhidi ya Senegal, kufuatia tukio la Senegal kufanya Paredi la ushindi wakiwa na kombe la AFCON 2025.

Morocco Yafungua Kesi FIFA Dhidi ya Senegal Kuhusu Kombe la AFCON 2025Mgogoro huo umetokana na hatua ya Senegal kuonyesha hadharani kombe hilo licha ya Shirikisho la Soka barani Afrika kutangaza awali kuwa Morocco ndio mabingwa rasmi kutokana na mchakato wa kisheria unaoendelea. “Kitendo hicho ni dharau kwa mamlaka za soka na kinachochea uhasama usio wa lazima,” ilieleza taarifa kutoka upande wa Morocco.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Morocco Yafungua Kesi FIFA Dhidi ya Senegal Kuhusu Kombe la AFCON 2025Morocco inasisitiza kuwa hatua ya Senegal ni kinyume na taratibu za kimataifa za soka, na inaitaka FIFA kuchukua hatua kali za kinidhamu. “Tunatarajia FIFA ichukue hatua madhubuti dhidi ya vitendo vya uchochezi na kutofuata sheria za mchezo,” iliongeza taarifa hiyo.

Sakata hili linakuja wakati ambapo Patrice Motsepe anaendelea na juhudi za kuleta maridhiano kati ya mataifa hayo mawili, akisisitiza mshikamano wa Afrika kupitia soka. Hata hivyo, hatua ya Morocco inaonekana kuongeza joto la mgogoro huo.

Morocco Yafungua Kesi FIFA Dhidi ya Senegal Kuhusu Kombe la AFCON 2025Kwa upande mwingine, shinikizo linaongezeka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa CAF, Samson Adamu, ambaye anaingia madarakani katika kipindi kigumu kinachohitaji maamuzi ya haraka na ya busara. “Hili ni jaribio kubwa kwa uongozi mpya wa CAF katika kusimamia migogoro ya aina hii,” amesema mchambuzi mmoja wa michezo.

Morocco Yafungua Kesi FIFA Dhidi ya Senegal Kuhusu Kombe la AFCON 2025Wadau wa soka barani Afrika sasa wanasubiri kwa hamu hatua ya FIFA pamoja na maendeleo ya kesi hiyo, huku wengi wakihofia kuwa mgogoro huo unaweza kuathiri taswira na umoja wa soka la Afrika endapo hautapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.