Walikuwa juu sana kwenye soka la dunia 1996 wanabeba EURO pale Wembley kwa kumfunga Jamhuri ya Czech, kisha 1997 Borussia Dortmund anaenda kubeba UEFA, 2002 wanacheza fainali kombe la dunia
Ujerumani ilikuwa kwenye ubora wa hali ya juu sana lakimi taratibu ikaanza kuanguka, 1999 Bayern anakosa UEFA, 2000 wanafanya vibaya EURO, kisha 2004 ikawa mbaya zaidi EURO, ukaja mjadala wa kitaifa sasa
Wanafamilia wa soka, wadau na serikali walikutana Hennes Weisweller ni academy kubwa hii karibu tu na Mji wa Bonn 2004, kuandaa mpango kazi wa Ujerumani mpya na kuifanya itawale soka la Dunia tena
Kipindi hicho Mkurugenzi wa Ufundi ni Robin Dutt, wakapitisha mpango wa miaka 10 wakiamini kufikia hapo matunda yaanze kupatikana Kisha waje na plan nyingine tena ya miaka 10, wakaanza kwenye soka la vijana
Academy zaidi ya 300 zikaanzishwa nchi nzima huku Kocha wa timu ya taifa Jurgen Klinsmann akiwa msimamizi Mkuu na mtaala wake maalum ambao academy zote wanaufuta (centralised philosophy) wakizalisha vipaji zaidi ya 650,000
Wakaja kuwekeza kwa Makocha wazawa pia, hii academy ya Hennes Weisweller ikawa ni sehemu ya kuzalisha Makocha hao, ikiaminika ni sehemu ngumu zaidi kwa Makocha kuhitimu, Makocha wanasoma masaa 800 kuhitimu huku England ni masaa 200.5 tu
Wahitimu moja wapo wa Pro Licence ni Julien Nagelsmann na Domenico Tadesco, leo hii Ujerumani ina Makocha wenye leseni B 28,400, leseni A 5,500 na Pro Licence 1,000 kwa takwimu tu za 2013, hii iliwalipa zaidi kwenye Scouting network walivuna vipaji vingi sana
Ule mpango wao wa miaka 10 uliwalipa sana ndani ya miaka nane, Ujerumani ana Kombe la dunia 2014, Semis Euro 2016, Kombe la mabara 2017, U21 Champions, U19 Champions na Fainali nne za U17, huu ndio ulikuwa mpango kazi wao ukatimia kama walivyotaka
Jana Ujerumani kapoteza lakini sio stori, wameanza mpango kazi wa miaka 10 ya pili, ndio kwanza mwaka wa sita huu kuna kitu wanajenga, tuwape muda wataamka tena, ikiwemo ujio wa Kocha mpya kama Nagelsmann, Hans Flick au Thomas Tuchels, ni suala la muda wamejiandaa ndio maana hawastuki
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



zeiyana
Ni kweli kama watajipanga hipasavyo bado wana nafasi kubwa ya kuilinda historia yao UJERUMANI
felister
wakijitahidi wataweza kuilinda historia yao
Povel
Germany ni Kama vile wamepoteah kwny soka hv lakin namatuin soon wanawez kurud kwny ubora tuliouzoeha katika soka la ushindani ulaya pamoja na dunia kwa ujumla
magdalena
ujerumani bado ina wakati mzuri tu wa kukitengeneza kikosi na kuwa katika msitari mzuri kikubwa ni juhudi tu
neema hassan
Asante kwa habar za michezo na burudan#meridian bettz
Shakila mrope
🙏🙏🙏
Fatina mfingi
Wajipange vizur ujeruman!
Ester jackson
Ujerumani wanaweza kama watakuwa wanajiandaa vema kuwakabili wapizani
Angelina
Goodupdate
Sauda
Wakiongeza juhudi watafanikiwa.
Samira
Ujerumani inabidi waongoze juhudi sana kwani timu kubwa kufungwa 6 ni fedheha sana
Lydia Emmanuel Magoti
Ujeruman ipo vizuri inajua nainaweza kukabiliana natimu hilio mbele yao siwapingi kwailo
Caroline
Ujerumani mnakwama wapi
Rahma
Waongeze tu juhudi watafanikiwa vizuli
Saupha mohamed
Good news
Fatuma kasomo
Wajitahidi tu
aisha
Wakaze sana ili wafanikiwe
Sabrina
Jitihada zao tu ndio zinahitajika
Janeflora malisa
Safi
David Pere
Germany ni Kama vile wamepoteah kwny soka hv lakin namatuin soon wanawez kurud kwny ubora tuliouzoeha katika soka la ushindani ulaya pamoja na dunia kwa ujumla
Issa
Itakaa swa timu ni kipind cha mpito
Tahiya
Wakat wao umepita