Cafu, Kutoka Sao Paulo hadi Palmeiras

Jina lake halisi ni Marcos Evangelista de Morais. Cafu ni kifupisho cha Cafuringa, jina la nyota wa zamani wa Brazil ambaye alifananishwa naye. Utotoni alikataliwa na vilabu vya Corinthians, Palmeiras, Santos, AtlΓ©tico Mineiro na Portuguesa kujiunga kwenye akademi zao.

Akakubaliwa na klabu ya Sao Paulo ya jiji la Paulista, ambayo ilimpa nafasi hadi alipoiva kuitumikia timu kubwa. Mwaka 1994, akauzwa Hispania klabuni Real Zaragoza. Hata hivyo, Sao Paulo wakaweka kipengele kwenye mkataba kinachoizuia Zaragoza kumuuza mchezaji huyo kwa timu yoyote ya Paulista.

Kuvunjwa kwa kipengele hicho kungesababisha faini ya dola milioni 3.6. Hii ni kwa sababu Sao Paulo walihofia Cafu asije akauzwa kwenye timu pinzani ya jiji lao halafu silaha ikawa imeuzwa kwa adui kama ilivyotokea kwa mlinzi Antonio Carlos.

Hofu yao kubwa ilikuwa klabu ya Palmeiras ambayo wakati huo ilikuwa na udhamini mkubwa wa kampuni ya maziwa kutoka Italia, Parmalat. Viwanja vya mazoezi vya Sao Paulo na Palmeiras vinatenganishwa na ukuta mmoja katika kitongoji cha Barra Funda…unaweza ukaona wangetesekaje!?

Na kweli, mwaka 1995, Palmeiras wakaingia tamaa ya kumnunua Cafu, lakini wakakutana na kile kipengele…ngoma ikawa ngumu. Matajiri wa Parmalat wakatafuta namna ya kumpata Cafu, wakaongea na klabu ya Juventude ya mji wa Caxias do Sul, ambayo ndiyo ilikuwa imepanda daraja.

Wakaitumia klabu hiyo kumnunua Cafu, akacheza msimu mmoja halafu akaenda Palmeiras.

Hii iliwauma sana Sao Paulo ambao walihisi uhuni umefanyika dhidi yao. Wakapeleka kesi mahakamani. Mahakama ikaipata Palmeiras na hatia na ikaihukumu ilipe faini ya dola milioni moja kwa Sao Paulo.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.Β 

Cheza sasaΒ 

Samurai Ken Online Casino

23 Komentara

    Marcos yupo vizuri sana

    Jibu

    Yupo vizuri anajua

    Jibu

    Morais Ni nyota na Yuko sahii

    Jibu

    Marcos ni kijana mahili sana

    Jibu

    Kijana anajitahidi sana

    Jibu

    Cafu anagombaniwa basi yupo vizuri

    Jibu

    Safi kijan piga kazi

    Jibu

    Namkubali

    Jibu

    Yupo vizuri anajua

    Jibu

    Kazi kazi anajiweza

    Jibu

    Kijana yupo vizuri

    Jibu

    Yupo vizuri sana

    Jibu

    Anajitahidi

    Jibu

    Nasubiri kurasa zijazo za habari hii ya mtu mbadi Cafu

    Jibu

    Cafu Kama cafu yupo vizuri

    Jibu

    anajitahidi

    Jibu

    Ndio kazi ya mpra hiyo

    Jibu

    Kijana mambo yak ni mazur

    Jibu

    kijana yupo makini sana

    Jibu

    Kijana yupo vizuri

    Jibu

    meridian unatupa habari za wachezaji ambazo tulikua hatuzijui safi ongera sana tunasubiri muendelezo wake

    Jibu

    Cafu ni hatari Sana

    Jibu

    Cafu ni mtu hatar Sana kwny ubora wake

    Jibu

Acha ujumbe