Mwamuzi kijana Ramadhan Kayoko amechaguliwa kuamua mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaopigwa Oktoba 23 siku ya jumapili utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kayoko ni mwamuzi kijana mwenye baji ya Fifa na miongoni mwa vitu vinavyompa hadhi ya juu kukabidhiwa mitanange mikubwa bila kusahau uweledi ambao akiuonesha katika michezo ambayo akichezesha.
Refa huyo ni miongoni mwa marefa bora katika ligi kuu ya Nbc licha ya umri wake kua mdogo ila amekua akionesha ubora katika michezo ambayo amekua akiichezesha ndo maana bodi ya ligi imemkabidhi mchezo huu mkubwa.
Refa huyo inakua sio mara ya kwanza kuchezesha mcheza wa watani wa jadi ameshawahi kufanya hivo kwani hii itakua mara ya tatu kwani ameshawahi kufanya hivo mwaka Julai 2020 kwenye mchezo wa nusu fainali ya Azam Federation uliozikutanisha timu pia mchezo wa ligi kuu September 2021.
Mchezo huo umekua wenye presha kubwa kuanzia wachezaji, mashabiki, mpaka kwa waamuzi hivo inahitaji mwamuzi alietulia na kuweza kuzitafsiri sheria za mchezo vizuri ambapo bodi ya ligi wamemuona Kayoko ndio mwenye uwezo huo.

