Watakaoikosa Kariakoo Derby Hawa Hapa

Kariakoo Derby: Kuelekea mechi kubwa ambayo husimamisha nchi kwa dakika 90, na sio nchi tu bali kwa wapenda soka wote hawatasubiri kusimuliwa, mtoto hatumwi dukani muda huo.

Makocha wa timu zote wamezungumza na waandishi wa habari, kabla ya mchezo muhimu na mgumu zaidi kwenye Ligi kuu, na hivyo kuzungumzia hali za wachezaji wa timu zote mbili zikoje kuelekea mchezo huu.

Kocha wa Yanga Nasradine Nabi amebainisha kuwa wachezaji wote wa klabu hiyo wako vizuri, isipokuwa wachezaji wawili ambao wataukosa mchezo huo, wachezaji hao ni Bernard Morrison na Salum Abubakar Sure Boy ambaye ametoka kuumwa Malaria hiyo huenda akacheza au asicheze itategemea na mazoezi ya leo.

 

Watakaoikosa Kariakoo Derby Hawa Hapa

“Morrison hatocheza kutokana na adhabu yake ya kufungiwa mechi kadhaa, mwingine ni Sure Boy ambaye ametoka kuumwa na Malaria, yeye itategemea hali yake itakuaje kwenye Mazoezi leo Jioni” Alisema Nabi.

Kwa upande wa kocha wa Simba Juma Mgunda amesema kuwa maandalizi kwa upande wao yako vizuri na wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo.

“Shomari Kapombe hatokuwepo kwa mchezo wa kesho kwa sababu ya majeruhi ila ameanza mazoezi, mwingine ni Jimmyson Mwanuke hawatakuwepo kwenye mchezo huu” Juma Mgunda

 

Watakaoikosa Kariakoo Derby Hawa Hapa

Kuhusiana na klabu ya Yanga SC kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Nabi amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo na kusema kuwa hiyo haina atahri kwenye mechi ya kesho.

Acha ujumbe