Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Mateu Alemany anaamini kuwa hali ya mkataba wa Ousmane Dembele inahitaji kutatuliwa haraka.
Vilabu kadhaa viripotiwa kuihitaji huduma ya staa huyu wakiwemo Manchester United na Liverpool, wakati staa huyu akitaka kusalia Barcelona.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 24 mkataba wake wa sasa Camp Nou unamalizika Juni na sasa yuko huru kusaini mikataba ya awali na vilabu vya kigeni.
Wawakilishi wa Dembele wamefanya mazungumzo na uongozi wa Barcelona kwa miezi kadhaa, lakini jinsi mambo yalivyo, Mfaransa huyo anatazamiwa kuwa mchezaji huru msimu ujao wa joto.
Akizungumza na Sport, Alemany alisema: “Dembele anajua vyema kile klabu inachofikiri. Ana ofa yetu mezani na anajua kwamba tunapaswa kutatua hali hii haraka. Tunatumai kuwa inaweza kuwa nzuri ikiwa atabaki nasi kwa sababu ni mchezaji muhimu na kutakuwa na taarifa hivi karibuni.”
Wakala wa Dembele, Moussa Sissoko, amedai kuwa mkwamo wa winga huyo wa mkataba na Barca hautokani na sababu za kifedha, na badala yake amependekeza kuwa uongozi wa Xavi umefanya mazungumzo kuwa magumu.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA