Michuano ya Kombe la Dunia imemalizika nchini Urusi, lakini licha ya mchezo huo kuwa na ufuasi mkubwa, ni wachache sana ambao hutafakari kuhusu chanzo cha mchezo huu maarufu.
Suala hilo la ni nani ndiye mtangulizi liliibuka mwezi Oktoba mwaka 2016 baada ya Rais wa China Xi Jinping na wahusika wa soka nchini Uingereza kukutana wakati rais huyo alipozuru uwanja wa Etihad nchini humo. Rais Xi ni shabiki wa Manchester United.

Ingawa pia Uingereza imekuwa ikijinadi kuwa waanzilishi wa mchezo huo, na hata timu yake ya taifa kujitungia wimbo wa mpira ‘unarejea nyumbani’ (It’s coming home) walipoandaa kombe la mataifa bora bara Ulaya na mwaka huu wakawa wanaiba tena wakati wa Kombe la Dunia ambapo walimaliza wa nne baada ya kushindwa na Ubelgiji 2-0 mechi ya kuamua mshindi wa tatu, baadhi ya wataalamu wanakiri China ndilo chimbuko la soka.
Kevin Moore, Mkurugenzi wa makumbusho ya kitaifa ya soka nchini Uingereza anakubali hilo.
“Ingawa England ndiyo chimbuko la mpira wa soka wa kisasa kama tuujuavyo, tumekuwa tukikubali kwa muda mrefu kwamba chimbuko halisi la mpira huu ni China,” alisema Moore, akiwatembeza Xi na Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo David Cameron.
Baadhi ya taarifa hudokeza kwamba mchezo unaokaribiana na kandanda ulikuwa unacheza visiwa vya Uingereza kati ya karne ya nane na ya 19, ingawa kwa miitndo tofauti inayokaribiana na raga.

Soka ya Shrovetide kama ilivyofahamika wakati huo ulikuwa mchezo wa umati usiokuwa na sheria kamili. Njia zozote zingetumiwa kuhakikisha mpira unafika ulikotakikana, bora isiwe mauaji.
Jina ‘football’ linadaiwa kuwa na asili ya Anglo-Saxon katika maeneo ya Kingston-on-Thames na Chester. Hadithi moja husema mchezo wa kwanza ulichezewa hapo kwa kutumia kichwa cha mwanamfalme wa Denmark ambacho kilikuwa kimekatwa kutoka kwa mwili wake baada yake kushindwa kwenye vita.
Derby, inaaminika kwamba asili yake ni katika kusherehekea ushindi wa vita karne ya tatu dhidi ya Warumi. Lakini hakuna ushahidi wa kuthibitisha hayo. Kabla ya uvamizi wa wanajeshi kutoka Normandy, hakuna ushahidi wowote wa mchezo kama huo. Kuna hadithi nyingine inayosema mchezo huo wa umati ulikuwa unachezwa pia maeneo ya Ufaransa, hasa maeneo ya kaskazini ya Normandy na Brittany hivyo kuna uwezekano kwamba mchezo huu ulifikishwa England na wavamizi kutoka Normandy karne ya 11.
Itaendelea..
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Fatuma kasomo
Habari njm
Dorophina
Habari njema kwa wanasoka
aisha
Historia ya soka imeeleweka sana
Sauda
Soka limepamba moto..
Rose kapinga
Mambo ya soka hayoo!!
Sadick
Waingereza hijinasibu kuwa waanzilishi wa mchezo huu kwa bahati nchi nyingone ndio zimepata mafanikio#meridianbett
Caroline
Kombe la dunia nimelimisi
Adelta
Habari kwa wanasoka#meridianbettz
Mwajumah
Habari njema#Meridianbettz
Nasra
Kumekucha tenaa
Agness
Asantee kwa taarifa meridian
Neema
Mambooo yaukwelii hayoo tumeyamic
JULIANA WILBARD ALEX
Da! Kumbe, asante kwataharifa
magdalena
soka inazidi kupamba moto kila kukicha
Fatina mfigi
Mambo mazur
Antony Luseno
Wanzalishi wa mchezo huu waliwaza mbali sana
Shani
Soka ni mchezo ambao unaleta hamasa sana kuliko michezo yeyote
rama
kweli soka lina historia sana
Mwanahamisi
Mambo mazuri
Rehema
Bonge la makala
Hidaya
Habari njema kwa mashabiki wa mpira
Janeflora malisa
Ni powa kbs
Amiri Kayera
Aah saf Kwa makala nzur
Saupha mohamed
Soko imepamba moto
Gabriel
Historia ya Soka imekaa poa sana 👍
Issa
Soka ni mchezo unaoleta hamasa ulimwenguni
Elika
Hilo ndilo soka
Leonard
Habari nzuri
Hope mwaikuka
Imeeleweka sana
Theonestina
Habari njema
Ester jackson
Asante kwa nakala mana sikujua hilo
Flomena
Good news
Sabrina
Asante kwa kunijuza
Theckla
Makala nzuri
Edgar
Mqmbo mzuri
Samiah
Gud
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
Povel
Historian ya kibabe
Isaya massawe
Imekaa poa sana hii
Amani
History nzuri Sana sikuwahi kujua Apo mwanzo
Latifa juma mohamed
So nice story .
felister
historia nzuri
Lydia Emmanuel Magoti
Habari njema kwa Wana soka
Ernest
Asante Meridiabet kwa Makali nzuri, Imetulia sana hii
Furahav
Nimekubali
Tatu
History nzuri kwenye soka
Salma ngende
Asante meridian
Genia Sikaluzwe
Mambo mazuri
David Pere
Waingereza hijinasibu kuwa waanzilishi wa mchezo huu kwa bahati nchi nyingone ndio zimepata mafanikio
warda
Historia nzuri sana