Usajiri unaoendelea ndani ya kikosi cha Azam FC unawapa jeuri wachezaji wa klabu hiyo kiasi cha kubeza usajili ambao unafanywa na klabu zingine hususan Simba na Yanga ambao wamekuwa wakisajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania.

Azam FC, jana walimtambulisha kipa mpya wa timu hiyo Ali Ahamada kutoka nchini Comoro ambaye wao walimtambulisha kuwa aliwahi kucheza Ligue 1 ya Ufaransa kwenye klabu ya Tolouse na hilo ndilo limewapa jeuri zaidi Azam FC.

Azam

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC Thabity Zakaria (Zaka za Kazi) alitupa dongo kwa Yanga na Simba kwa kudai kuwa wao hawasajili wachezaji ambao walicheza Ulaya na wakashindwa na kurudi Afrika na kwenda kwenye timu zao, wao wanatoa watu huko kuja kwao.

“Sisi Azam FC, hatusajili wachezaji ambao walicheza Ulaya wakashindwa wakakaa nyumbani bila timu muda mrefu na kisha wakaenda kwenye timu zao. Tumesajili kipa kutoka Ulaya kwenye ligi ya Ufaransa.

“Ukiachana na huyo, wachezaji tuliowasajili walikuwa wanagombewa na klabu kubwa Ulaya ila Azam ikashinda vita na wakaja kwetu.”

Azam hadi sasa imetambulisha wachezaji saba, watatu wakiwa wakiwa kutoka ndani na wanne wakimataifa kutoka mataifa mbalimbali. Wachezaji wa ndani ni Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji.

Abdul Suleiman Sopu kutoka Coastal Union na Nathaniel Chilambo kutoka Ruvu Shooting. Wakutoka nje ya Tanzania ni Kipre Manou kutoka Ivory Coast, Tape Edinho kutoka Ivory Coast na Issah Ndala kutoka Nigeria.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa