VAR- Haki Inavyopoteza Radha ya Soka

VAR ni kifupi cha neno la kingereza lenye maana ya Usaidizi wa Muamuzi kwa Njia ya Televisheni, Hii imekua kawaida sana kwa kipindi cha karibuni kwa waamuzi wa michezo ya kimataifa kutegemea maamuzi ya VAR kutokana na Mwamuzi wa kati na wasaidizi wake kushindwa kung’amua kosa litakaloendelea wakati mchezo ukiendelea. Matuzimi ya VAR yamekua na Faida kubwa hususan kwenye zile timu zinazotegemea zaidi maamuzi ya haki katika mechi lakini kwa namna kubwa sana imeleta kupooza na kupunguza ile radha ya soka hususan kwenye matukio ya kusisimua kwenye soka.

Mwaka 1986 kwenye mashindano ya Kombe la dunia lililofanyika nchini Mexico katika uwanja wa Estadio Azteca katika jiji la  Mexico City Diego Armando Maradona alifunga Goli la mkono lililojulikana kama Goli la mkono wa Mungu, Goli lililoipaTaifa la Argentina heshima kwa kumfuna Muingereza goli 2-1, Sasa tukirudi kwa miaka ya kileo, miaka ya utandawazi , miaka ambayo waamuzi wanasaidiwa na teknolojia kufanya maamuzi Goli lile la Argentina lisingeitwa Goli na ingebaki kwenye historia kua hakukuwahi kua na goli la namna ile.

Goli la Mkono la maradona

Kama hiyo haitoshi VAR imekua ikiwafanya wachezaji wengi kuingia kwenye Adhabu ambazo kwa tekniki za mpira ilikua ni kawaida kutokea, mfano zamani mpira unaweza kugusa mkono na Muamuzi hajaona basi ni bahati ya timu iliyozuia kuendelea na soka na inafanya hali ya wachezaji kushambulia na kuzia kua kubwa na morali. Sasa hivi unaweza kufunga goli ukaanza kushangilia kwa kuvua Jezi yako ukajikuta umekula kadi ya Njano na goli lika kataliwa.

 

 

2 Komentara

    Great content

    Jibu

    #TimuYaUshindi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.