Kylian Mbappe amesema kwamba alijiunga na PSG ili aweke historia kwa kushinda taji la Champions League katika mchezo wa kukamilisha msimu dhidi ya Bayern Munich.
PSG iliyowatoa RB Leipzig katika hatua ya nusu fainali na kufanikiwa kufika fainali yao ya kwanza katika Champions League itakutana uso kwa uso na mabingwa wa Bundesliga mjini Lisbon siku ya Jumapili.
Mbappe alishawahi kufika hatua ya nusu fainali akiwa na timu ya Monaco mwaka 2017 kabla hajafanya uhamisho wa pesa nyingi na kutua PSG.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ameonekana kuwa vizuri baada ya kupona jeraha lake la kifundo cha mguu na ameamua kuhakikisha PSG inashinda mashindano hayo makubwa ya Ulaya kwa mara ya kwanza wikendi hii.

“Sisi ni ‘underdogs’ kulingana na kila mtu anavyotuchukulia na tunapenda tukisikia hivyo. Nilicheza kwenye Fainali ya Kombe la Dunia na nilishinda. Sasa hili ni taji lingine kubwa ambalo ninataka kushinda kwenye maisha yangu. Nitapambana kama ni siku ya mwisho ya maisha yangu.
“Naamini tuna ubora sawa na Bayern Munich. Endapo Ikicheza mchezo wa kutumia nguvu, sisi pia tutakuwa na nguvu sana kuona ikiwa watapenda ladha ya dawa yao wenyewe.”
“Tuna Kocha Mjerumani ambaye anajua mbinu za Kijerumani. Anajua jinsi ya kuwashughulikia Bayern Munich.”
“Hii ndiyo sababu kwanini nipo hapa,” Mbappe aliongea na waandishi siku ya Jumamosi. “Mara nyingi nimekuwa nikitaka kuandika historia katika mpira wa Ufaransa, sasa nina fursa ya kufanya hivyo.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


JULIANA
Asante kwataharifa
Furahav
Litakua jambo zuri sana km leo utafunga na kuchukua ubingwa.
Antony Luseno
Ndoto yake Leo usiku yaweza kutimia
Sabrina
Mbappe atafanikisha tu hitajio lake la kuchukua ubingwa wa champions league asiwe na papala anatakiwa ajitume
Zeiyana
Hizo ndoto zake mbappe lakini sio kwa timu wanayo kuna nayo..!kwa Bayern munch sio kilaisi laisi hivyo yani mjipange sana
aisha
Mbappe tunakuombea ukamilishe ndoto yako leo kila la kheri brooo
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri mbappe adi yako itatimia mpambanaji
Ernest
Binafsi nafurahi kuona kila mchezaji anajitoa Asilimia zote kuweza kutimiza ndoto yake, Leo utakuwa usiku mzito sana Barani Ulaya.
marry
yuko vzr sana
Sadick
Tunasubiri kuona maneno yake yanatafsiriwa kwa vitendo Ushindi hautakuwa rahisi kwa yeyote#meridianbettz
Christa
Na Leo itabidi aikamilishe historia
Nasra
Ajitahidi atatimiza alichokusidia
Ester jackson
Good news
Mwanahamisi
Yuko vizuri
Amiri Kayera
Sasa ni wakat kuvunja record bahat haiji mala 2
Sauda
Aongeze juhudi atatimiza malengo yake
Adelta
Mbappe Yuko vizuri na anajiamini ktk majukumu yake @meridianbettz
Issa
Anajipa imani tu bayern ni moto na champion league wanalisaka patachimbika leo
Caroline
Leo onyesha umahiri wako
Mwajumah
Na leo usiku itabidi akamilishe historia#Meridianbettz
felister
timiza ndoto yako basi
Dorophina
Leo mbappe ndio siku ya kuwaonesha Wana psg Mambo makubwa
Tatu
Mbappe kujiunga na PSG ni jambo LA msingi tena hukovatakuza kipaji
Khadija
Good new
Hope mwaikuka
Timiza ndoto zako
jullie
yuko vizur sana
Povel
Ngoj tuone Kama dreamx can true leo kwa mbappe
Samira
Kiukweli mbappe ni mchezaji mzuri sana
Shafii
Kila mchezaji hua anandoto katika career yake nadhani mbape ndoto yake ilikua hii.
Neema
Ndoto zake zitatimia siku hadi siku
Saupha mohamed
Mbappe yupo viziri
Latifa juma mohamed
Talent and famous player kila la kheri ktk ndoto zake.
warda
Ndo basi tena mmesha pigwa#Meridianbettz
rama
Maoni:safiii sana
magdalena
mbappe ndoto zake hazikufanikiwa kutimia baada ya kupokea kichapo zidi ya bayern
Salma ngende
Vizuri
Gabriel
Itabid aendelee kuwa na ndoto hizo maana bado kijana huyo
Rose kapinga
Kujiamini ndio mpango mzima!!!
David Pere
Mbappe alishawahi kufika hatua ya nusu fainali akiwa na timu ya Monaco mwaka 2017 kabla hajafanya uhamisho wa pesa nyingi na kutua PSG.
farida ahmadi
Mbape Yuko vzr Sana
Rehema
Yuko vizuri
Tahiya
Usijar kijana kaza buti utatimiza ndoto yako
Samiah
Yuko vzr