Australian Open 2022: Osaka Anawaka!

Wakati headlines za Djokovic vs Serikali ya Australia zikiwa zimetamatika, mashindano ya Australian Open 2022 yameanza rasmi leo. Naomi Osaka ameanza kwa kishindo.

Bingwa mtetezi wa Australian Open (wanawake), Naomi Osaka, ameyaanza vyema mashindano ya mwaka huu kwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza. Osaka alikuwa uwanjani kuchuana na Camila Osorio mchana huu.

Osaka alianza vyema mchezo kwa kuongoza kwa matokeo ya 5-0 kabla ya Osorio kupindua meza. Uwepo wa mashabiki uwanjani, ubora binafsi na upinzani kutoka kwa Osorio, vilimuongezea ari Osaka ambaye alirejea tena kwenye nafasi ya kuongoza na kumaliza mchezo kwa seti 6-3 6-3.

Wakati Osaka akiibuka kidedea, kwa mara ya pili mfululizo, Sofia Kenin anayaaga mashindano kwenye hatua za mwanzo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Madison Keys. Kenin ambaye alikuwa bingwa wa Australian Open 2020, amejikuta akiambulia kipigo na kutolewa mapema kwenye mashindano ya mwaka 2021 na 2022.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe