Van Persie Alivyowaliza Wahispania Kwa Goli la Kupaa Angani

Si unakumbuka Giovanni Van Broickhoist alivyoisimamisha Afrika Kusini ile 2010. Wahuni wa Soweto wakakubali kuzima misokoto, wakasimama kutazama matusi yasiyokera ya ‘m-dutch’. Lile bao, hadi madaktari walisahau kuwasikiliza wagonjwa wao.

Vipi kuhusu Arjen Robben mbele ya wahispaniola 2014 pale Brazil? Namna alivomzunguka Sergio Ramos, kisha kumzalilisha Iker Cassilas, lile ni kosa la jinai. Mabao kama yale yanaweza kukunyanyua kwenye ‘kibanda umiza’, Ukarudi kulipa mara ya pili.

Tuachane na hayo. Unamkumbuka ‘superman’ Roben Van Persie? Ile siku Hispania wanakufa 5-1 pale ‘Arena Fonte Nova’. Ilikuwa mara ya kwanza Hispania wanafungwa zaidi ya mabao manne katika mchezo wa kimashindano tangu 1963. Van Persie alifunga bao la kwanza.

Hispania walikitawala kipindi cha kwanza. Penalty ya Xabi Alonso iliwaweka mbele dakika ya 27. Dakika mbili tu kabla ya mechi kwenda mapumziko, David Silva alishindwa kuitendea haki pasi ya Andres Iniesta, akaamua kuubetua mpira badala ya kutulia azisake nyavu za chini za Jasper Cillessen.

Baada ya kona ya David Villa kutokuzaa matunda kwa Hispania, mpira ulisukumwa katikati ya dimba, ikawekwa pasi moja kushoto mwa uwanja kwa Daley Blind. Wakati huo Van Persie yupo katikati ya Jordi Alba na Sergio Ramos.

Van Persie akaagiza krosi iletwe ndani ya box. Kwa kuwa Gerad Pique alikuwa amemshika Arjen Roben, alimuweka Van Persie ‘onside’. Wakati huo Ramos alifanya kosa la jinai kumuacha Van Persie nyuma yake. Casillas akatoka kuja kumlaki, Van Persie alitoka na kichwa kimoja bora sana kwenda nyuma ya wavu wa Iker Casilas.

Namna alivopunguza kasi ili aukute mpira, namna alivopaa na namna alivoupima urefu wa golkipa na goli. Ni kama unaangalia uongo wa superman, spiderman na batman kwa pamoja. That goal was more than sensational.

40 Komentara

    Hilo lilikuwa goli Bora la mashindano kwa upande wangu mimi

    Jibu

    Da hili goli lilishangaza wengi

    Jibu

    Goli hilo lilinishangaza sana

    Jibu

    Hilo goli lilikuwa la kipekee na la kihistoria.

    Jibu

    Van mchezaji mzuri

    Jibu

    dah naikumbuka sana ile siku n ya kihistoria kwa kwel

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Roben alikuwa mwamba akiwa uwanjani alikuwa hana mpinzani

    Jibu

    Lilikuwa Gori la mwaka

    Jibu

    VanPersie Amepotelea wapi jamani #Meridianbettz

    Jibu

    lile bao hadi madaktari walisahau kuwasikiliza wagonjwa wao

    Jibu

    Ilikuwa hatari sana mm mwenyewe nilishangaa sana#meridianbettz

    Jibu

    Ilikuwa goli la kihistoria

    Jibu

    Iilikua ni goli la ajabu san

    Jibu

    Van alikuwa mchezaji bora na mwenye nidhamu akiwa uwanjan namkubal sanaa na goli zuri

    Jibu

    Kwenye lile kombe la Dunia hili goal la VAN PERSIE ndio lilikuwa Goal bora la mashimdano kwasababu lilikuwa lakipekee sana nikashangaa eti akapewa mtoto James na bao la kawaida sana

    Jibu

    Mtu aliyekuwa na uwezo wa kufunga unpredictable goals,van persie

    Jibu

    Goli la maajabu kwa kweli

    Jibu

    Huyo mchezaji ni hatari#meridianbetz

    Jibu

    Hii diving header ya Van Persie utasema kapiga na mguu!!!

    Jibu

    Nakumbuka goli Hilo la van persie
    Likuwa goli Bora la mashindano.. Enzi zake huyu jamaa alikuwa noma Sana#meridianbettz

    Jibu

    Aisee nlkua cjui hii

    Jibu

    Arsenal walipoteza bahat kumuacha van persie aondoke

    Jibu

    Hapo ndio wapenzi wa mpira tunasuuzika na roho. Hakuna maumivu ya kiingilio bali raha moyoni. Van persie alijitoa mzimamzima#meridianbettz

    Jibu

    Lilikuwa bonge la goli

    Jibu

    Huyu jamaa hatari,mana alipaa kama kunguru kufunga goli.

    Jibu

    Hili goli unbelievable kwa jins lilivyo fungwa van persie alikua straker wa aina yake

    Jibu

    Van persie top striker kwngu mm yupo vzr nakumbuk mbal sana goli lake thnks meridian kwa update

    Jibu

    Alitisha sana

    Jibu

    Van persie atarii kwasababu aliwashangaza watu kwakombola alilolitoa mtuatarii Sana huyo

    Jibu

    lilikuwa goli Bora la mashindano# meridianbettz

    Jibu

    Fundi huyo

    Jibu

    Duuh jamaa ni noma alishangaza kwa kweli

    Jibu

    Van ni mchezajiii mahirii sana kaacha historia

    Jibu

    Lilikuwa bonge moja la goli aisee

    Jibu

    Huyo jamaa ni fundi wa mpira

    Jibu

    Tnx meridian makala nzuri nilikuwa sifahamu chochote

    Jibu

    Huyo jamaa ni fundi

    Jibu

    Hilo goli lilikuwa hatari hakuna shabiki aliye kaa chini

    Jibu

    Van perse ni mchezaji bora na mzuri Sana hongera Sana kwa goli zuri kama hilo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.