Kipa namba moja wa Yanga Djigui Diarra ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Singida Big Stars kwa kuwa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Mali.
Mdaka mishale huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi hivyo kwa sasa amebakiwa na nyota wawili ambao ni Aboutwalib Mshery na Erick Johora.
Pia Aziz KI naye atakosekana kwenye mchezo huo anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi ukiwa ni mchezo wake wa pili.
Cedric Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
“Mchezo utakuwa mgumu tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo ili kupata pointi tatu muhimu,”.
Singida Big Stars imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba inakutana na Yanga iliyotoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.