Barcelona walikuwa wanaongoza mbili kwa moja dhidi ya Chelsea. Hapo John Terry ametolewa nje mapema sana. Kumbuka mechi ya kwanza darajani Chelsea walishinda kwa bao pekee la Didier Drogba. Kama ingeisha hivi, Chelsea walikuwa wanakwenda fainali ya UEFA.

torres

Lakini ilionekana kama ‘HAIWEZEKANI’ kwa Chelsea. Utawadhibiti vipi Barcelona kwa dakika 45 wasikufunge mkiwa pungufu??

Nikiwa katikati ya mashabiki wachache wa Chelsea, jamaa mmoja aliniambia, “Acha mashaka, Chelsea inakwenda fainali” Kusema ukweli, SIKUAMINI.

Si kwamba naishabikia Chelsea. Si kwamba nili-bet kwa Chelsea, bali nilitaka Chelsea watwae UEFA kwasababu ya mwanaume mmoja wa kiafrika, ‘DIDIER DROGBA’.

torres

Kwa miaka mingi niliishi nikimhusudu sana askari huyu. Niliishi nikihusudu mapambano yake na nilitamani sana afanikiwe kutwaa ndoo ya Ulaya.

Dakika ya themanini, Mwili wangu ukiwa unatetemeka kwa baridi, mkononi nimeshika tochi na mwamvuli wangu. Nazifikiria kilometa za kukanyaga kurudi nyumbani, tena mvua ikiwa inanyesha.

Roberto Di Matteo alimnyanyua Fernando Torres. Saa hiyo Chelsea wapo ndani ya box lao wote, wawazuia watoto wa Catalunya. Kumbuka Barcelona wanahitaji bao moja tu wasonge mbele.

torres

Kila mtu akiwa anazifikiria dakika za muda uliopotea, Didier Drogba ameshindwa kukaa kwenye kiti, amezuiliwa ili asiingie uwanjani.

Saa hiyo mashabiki wa Chelsea wamenywea! Si waliokuwa Camp Nou wala waliokuwa ndani ya vibanda umiza nyumbani Tanzania waliokuwa na nguvu ya kuzungumza.

Barcelona walipiga shambulizi, Chelsea walizuia na mpira ulioshwa mbele. Fernando Torres alikuwa mwenyewe katikati, kwasababu Barcelona walipanda mbele wote. Torres alikimbia na mpira kisha akamfuta golkipa Victor Valdes na kuweka mpira kambani.

torres

Chelsea wakatinga fainali ya Ulaya na Didier Drogba alikwenda kutwaa ndoo ya Ulaya.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

mini power roulette

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa